Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Idris | TROOPER #Ep 8

Mziki Mzuri
TROOPER
Mimi kama watanzania wengi sikuwa namfahamu Idris, mara yangu ya kwanza kumuona ilikua kwenye TV akiwa mmoja wa wawakilishi wa Taifa hili kwenye kipindi cha Big Brother mwaka 2014. Nilivyouandika hapa huo mwaka ndo imenigusa akilini kwamba ni miaka sita tu imepita toka Idris Sultan amekua kwenye macho na midomo yetu. Na pengine ataendelea kuwepo kwenye midomo na macho yetu kwa miaka mingi zaidi, kuna sehemu nilikua naangalia interview yake moja na alisema yeye umaarufu ndo kitu ambacho anakipenda zaidi, pengine na ndo maana alienda kwenye shindano la Big Brother Africa na toka ametoka mule kama mshindi sidhani kama kuna wa kumsimamisha au cha kumsimamisha yeye kuweza kutimiza ndoto yake hiyo.
Kama kijana mwengine yoyote toka tumfahamu Idris amefanya mambo mengi ya kutuonyesha kipaji chake, kuanzia vipindi vya radio na tv, ku mc shughuli mbali mbali, kufanya comedy na sasa kaamua kujikita kwenye uigizaji na hakuna swali juu ya kipaji chake cha uigizaji kama kimepamba moto ivi na pia inaonekana amenza kijielewa na sidhani kama kuna wa kumsimamisha.
Idris aliweza kushinda zile pesa za Big Brother ambazo zilikua ndo habari ya mjini, inawezekana pia zile pesa zilikua na Tanzania nzima maana nakumbuka hasa mahesabu yalokua anapigiwa baada ya ile hela ‘kuyeyuka’ katika mazingira ya kutatanisha kitu ambacho kilimfanya awe kama kichekesho cha nchi. Inachukua moyo wa ziada kuweza kupambana na mawe ambayo kijana huyu alikua anarushiwa kutoka kila kona ya kuhoji na kudhihaki maisha yake na baadhi ya maamuzi ambayo aliyafanya kwenye maisha yake. Na nadhani mpaka hapa tulipo? Idris 10 sisi 0! Nakumbuka kama miaka mitatu iliyopita nilikua na kikao nae sehemu akaniambia anashkuru sana haya sote yametokea kabla hajafikisha miaka 25, kwa yeye kuweza kufanya mistake kama alofanya nyuma haiwezi kutokea tena. Anaamini amejifunza mengi na kuyaona mengi baada tu ya kupitia mtihani ule.
Kwenye maongezi yetu haya tulikua hatuwezi kuacha kuzizungumzia pesa hizo ‘za taifa’ na kutaka kujua haswa kinaga ubaga juu ya nini haswa kilitokea. Pia kuhusu mahusiano ya kimapenzi yalowahi kutokea maishani mwake, vipi aliweza kupambana na mawe yaliyokua yanarushwa upande wake, humu pia tumezungumzia biashara michongo ya mjini, kipaji chake na mipango yeke endelevu pia. 
Here’s to our Trooper, tafadhali enjoy!