Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Gigy money | ZILE KHADITHI #Ep 12

Mziki Mzuri
Mara nyingi huwa tunahukumu watu ambao hata hatuwafahamu na pengine hatujawahi hata kuongea nao hata mara moja kwasababu tu ya muonekano wao au kwa kitu tumeskia wamefanya au wamesema, au kwasababu fulani kasema jambo fulani kuhusu yeye ndo hapo nasi tunajifanya tunawajua sana na kutoa hukumu zetu juu yao, kama vile tunawafahamu sana au tunajua sababu ya yote ambayo tumeona au kuskia tu wamefanya au kusema. Hayo ndo maisha ambayo mgeni wetu wa wiki hii amekua akiishi kwa miaka kadhaa sasa.
Jina lake ni Zawadi aka Gift, binafsi sikumbuki siku ya kwanza kukutana naye au kumsikia ila nakumbuka siku ya kwanza kusikia wimbo wake na kusema unajua nini, huyu kadadaa akituliza maskio yake basi anaweza kufika sehemu, akaja akatoa single nyengine, pia ilikua moto na mashairi na pengine sababu ya yeye kusema alichokua anakisema mule ndo kilinifanya haswa nijue ndani yake kuna kitu cha kupewa nafasi na uangalifu ili apelekwe panapotakiwa. Najua muziki kwa miaka ya hivi karibuni umekua ‘ukiingiliwa’ na vipaji feki na vya kulazimisha vingi tu na kila mmoja ana sababu yake ya kutaka kufanya hivyo. Mimi na wewe tunatakiwa kuheshimu kila hustle ya mwenzetu tunayoina au kukutana nayo maana mtu anakua anajaribu na kwa hilo tunastahili kuheshimu, haijalishi anafanya nini, kama kinakukera au kukufurahisha, as long as kinamfaidisha yeye na kumpa raha basi sisi tunatakiwa kuheshimu na ndo hiyo heshima tunatakiwa kumpa Zawadi pia.
Kikubwa kwa Gigy ni mdomo wake ambao kwa wengi wetu tunasema na kuamini hauna chujio hata kidogo. Haogopi kuongelea maisha yake ya binafsi na kwa hilo linajumuisha mahusiono ya ki mapenzi, mahusiano na Mama yake, rafiki zake, watu alokua nao na pengine hata kazi... Ila sasa ni kitu gani kinamfanya mpaka leo bado anapata ma deal ya kazi, ana marafiki wazuri, halali nje na anakula vizuri na mtoto wake anaishi vizuri tu?
Hiyo ndo sababu ya mimi haswa kutaka kukutana nae na kuongea nae kwa kiasi changu. Kipi haswa kilutufanya tumfahamu? Anadhani ubora wake uko wapi? Huwa anawaza kabla hajaongea? Kipaji chake anadhani ni nini? Mama yake ni mtu wa aina gani? Bintiye je alitokea wapi? Kuna mambo ya imani za kishirikina pia huwa yanaongelewa sana hayo nayo? Style yake ya maisha haimgharimu na masuala mengine ya maana kweli?
Majibu yako humu ya ile khadithi ulokua unazisikia kila siku mimi na wewe, yangu matumaini tutayapa yote. 
Tafadhali enjoy.

Follow:

Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown