Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Zuhura | DADAKE #Ep 13

Mziki Mzuri

Moja ya watu walopigana vita zao wenyewe kimya kimya na wengine wakashuhudia tu mtu yuko jukwaa la kimataifa na anazidi kusoga. Maana halisi ya nitafanya kama ilivyo ili tuone mbele itakuaje maana Mungu amekua mwema haswa, so kwake yeye hakuna kinachoshindikana na kiukweli kabisa kama wewe ni wa mbili basi utaendelea kuzivaa maana mwenye hizo mbili kuvaa moja abadan!
Mimi nilikutana naye kwa mara ya kwanza kwenye mahangaiko ya kazi yangu ya kwanza, radio mpya ilikua imeanzishwa hapa mjini, kwa msaada wa Soggy Doggy Anter aka Chief Rumanyika nikapata nafasi ya angalau kuingia mule ndani na nikakutana na watu kadhaa ikiwa pamoja na Zee A aka Zuhura Yunus huyu wa sauti tamu na lafdhi ya kutaka tu umskilze mwenye kuendesha ‘Dira ya Dunia” na siku za hivi karibuni “Focus on Africa” na hapo pia (sehemu tulokutana mara ya kwanza nami nilipata kazi yangu ya kwanza kama mtangazaji wa radio)
Hakuamka tu asubuhi akawa mtangazaji wa BBC, ila allipita kule na huku na kujiongeza ki elimu ndo mpaka leo yuko hapo. Umaarufu wake ukanza kujijenga kidogo kidogo na uwezo wake wa kuongea Kiswahili fasaha pia ukampa nafasi ya kuweza kupata kazi hiyo baada ya kuwa nchini Uingereza ili kujiendeleza na masomo, basi naam… Internship akaanza na baada ya hapo BBC wakawa wanaajiri mengine ndo stori tu kama nnayokupa hapa
Zuhura alikua katika mipango yetu ya kuweza kupata nafasi ya kukaa chini na kuongea nae mambo kadhaa ili wananchi wapate kumfahamu zaidi. Lakini msukumo pia ulikuja baada ya baadhi ya watazamaji na waskilizaji wetu pia kutaka kumfahamu zaidi na likawa ni moja kati ya majina yalokua yakitwajwa zaidi yawe kwenye kipindi chetu na haikua kesi kwetu hata robo maana mipango ilikua kama mitego ya ki Vietnam. Dadaake akajaa.
So yeye ni nani? Kwao wapi? Wazazi wake ni kina nani? Ana ndugu walozaliwa pamoja? Wako wapi? Lini alianza hiii kazi ambayo anaifanya na sisi inatuvutia sana? Shuleni je ni wapi? Khadithi juu ya yeye kujifunika ushungi? Alilazimishwa? Anatokea kwenye familia iloshika dini sana? Kazi yake ya kwanza ilikua ipi? Yuko na mtu anayemsaidia kufungua zipu ya gauni akirudi nyumbani kutoka ofisini huku akiwa kachoka sana? Sisi mwenzangu tuliuliza hayo yooote na zaidi. Ukiachana kwamba yeye ni mtangazaji hodari na mtu poa sana, ambaye anapenda tu kucheka masaa yote basi Zuhura pia ni performer mzuri tu wa mziki, anaweza kuimba, kuchana na kucheza, ila hiyo iwe siri yako mwenzangu.
Pia huyu ni mmoja kati ya yatu wanao ni inspire na kupenda zaidi kazi zao.
Cheers kwa Dadaake
 
Follow: