Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Darassa | KAWIA UFIKE #Ep 16

Ep. 16 - Salama Na Darassa | KAWIA UFIKE

Thabit Shariff Ramadhan my guy, siku zote mkimya, yupo kama hayupo, anayeona lakini humkuti anaangalia na mwenye kuyabeba yanayobebeka na kuyaacha ambayo hayapaswi kuchukuliwa, huyo ndo yeye na leo ukimuona mpe tu heshima zake, pengina si kwasababu kakuzidi umri, ila kwasababu aliyechelewa lakini KAFIKA.

Tena, sikumbuki lini ilikua mara ya kwanza mi naye kukutana ila nakumbuka nilipomuona 2016 mwezi wa 12 kwenye mazoezi ya show ya usiku ya Tuzo za Muziki za EATV, alikua wa mootoh, ukiachana na watu waliokua ndani ya game, hakuna aliyejua alitokea wapi, ila boom!! Kwenye sikio na kila mdomo wa wana Afrika ya Mashariki dunia kwa ujumla, kiiila mtu alikua anaimba MUZIKI wa (ya) Darassa.

Hapa atatuambia kwamba alikua kwenye game muda mbona? Ila muda wake tu ulikua haujafika (pengine ushaisikia hiyo story) ila ni kweli, muda wako kama Mwenyezi Mungu hajasema ndo huu basi inakua hata ufanyeje haufiki mjini. Imagine kuwepo toka enzi za ECT, Dully wakati wamooto, wakati Complex bado yuhai na Q Chief ana nywele zake zote kichwani na rasta juu lakini 2016 ndo akapata break yake kubwa ya kwanza sio mchezo. Kwa hilo pekee tunafaa tumpe salute zake.

Muziki haikua single yake ya kwanza, haukua wimbo wake wa kwanza kurekodi, haikua video yake ya kwanza aidha, ila kwa baadhi ya watu Darassa alikua ‘msanii mpya’. Hapa, tuliongea juu ya maisha baada ya MUZIKI, na kabla. Baada ni kwasababu lilikua ndo swali la kila mtu, kipi kilikosewa, nini kilitokea? Hakua na uwezo wa kutengeneza hit tena? Ilikua bahati tu ile? Na kabla ya hapo alitokea wapi haswa? Ali struggle kabla ya kupata mwanya? Shuleni ni vipi? Changamoto za kazi? Ana mtoto? Mke? Mwenza? Nani ni rafiki yake kwenye muziki? Subira haswa anayo? Alijifunzia wapi?

Majibu yako humu, tafadhali enjoy.Follow: