Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Madee | MPAKA MISHALE #Ep 18

Mziki Mzuri
Mara zote ukiwaza Manzese kama wewe ni mpenzi wa Bongo Flava basi utawaza Madee tu. Waliosema au alipojiita Rais wa kule sidhani kama kulikua na upinzani wowote, najua kulikua na mtu mwengine ambae alikua anataka hiyo title ila tayari ilikua na mwenyewe ambaye inamkaa haswa. Busara zake za miaka ya karibuni na haswa niseme zaidi mwaka huu ni moja ya vitu vilinivutia kutaka kuongea nae. Maana si mara nyingi kwa kijana ambaye amekulia maisha ya ‘ki gangster’ kuwaza watu wengine au hata kuonyesha kuguswa na kitu flani. Ili mtu afikie kufikiria suala la umri kwenda na kuanza kujijengea kwenye maisha ya baadae siku Muumba atakapotuita ni jambo ambalo tunatakiwa kujifunza kutoka kwake. Na pia ni moja ya idea maridhawa nimeskia mwaka huu. Na kubwa kabisa ni kuwa mimi na yeye hatukuwahi kuwa na maongezi ya aina hii, wakati muafaka kabisa... Seneda yeye haswa alizaliwa wapi? Ametokea kwenye familia ya mziki? Wazazi wake ni watu wa aina gani haswa? Kule Manzese ndo kwao? Au ilikua maskani tu? Na kama si hivyo aliwezaje kujikita mpaka akawa rais? Suala la elimu je? Wakati anakua kuna makashkashi yoyote alipitia? Na muziki? Na Babu Tale? Na Abdu Bonge aliwatoa wapi? Na TipTop Connection nayo chimbuko lake ni wapi? Niliongea naye kuhusu hayo na kuwa ‘chawa’ ili yake yamuendee kwenye suala zima la kujijengea empire yake... Muziki umemfanyia nini? Kama Baba ni kitu gani ambacho watoto wake wanapenda kuhusu yeye? Yuko na hao Mama za watoto wake? Ki ukweli kuna mengi tumezungumza naye lejendari huyu wa Bongo Flava ikiwa pia pamoja na wimbo wa ‘Pombe Yangu’ ambao nao pia una story yake ya kipekee. Yangu matumaini uta enjoy kama nilivyo enjoy mimi na wenzangu wakati tuna film hii.