Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Romy Jones | PLUG #Ep 14

Mziki Mzuri

Romeo boy handsome toka Kinondoni mpaka Tandale na sasa duniani kote. Ni kijana wa town, mcheshi, mtanashati, mwenye madevu na mcha Mungu, Ila pia ni Kaka yake mwanamuziki superstar toka Tanzania ambaye ni Diamond Platnumz. Mimi na Romy tunafahamiana miaka mingi, na kama ulivyodhani nilianza kumjua yeye kabla sijafahamiana na Nasib, story yetu inaenda toka enzi za ‘ujana’ wetu, rafiki zake ndo rafiki zangu na tulikua tukikutana karibia kila wiki. Toka Platnumz awe al maaruf Romy amekua nyuma yake siku zote, toka video ya kwanza ambayo umemtuambulisha kwetu super star huyu Romy alikuwemo pia kwenye video hiyo kama mume mtarajiwa wa msichana ambaye Platnumz alikua ndo mpenzi wake. Toka siku hiyo tumekua tukiwaona pamoja kila sehemu kama kope kwenye jicho. Miaka ya hivi karibuni sikuacha kugundua kwamba rafiki yangu huyu kabadili tabia, siye yule nlokua namfahamu wa miaka mitano iliyopita, kuanzia muonekano, kazi, jinsi anavyojibeba na hata maongezi yake. Pia nimekua nikimuona akifanya kazi ambazo si za bora liende na badala yake ni kazi ambazo zinasimama haswa na kujieleza zenyewe. Kwa mbali nilikua naangalia na nikasema kwanini haswa nisimtafute rafiki yangu huyu ili atuambie mimi na wewe siri haswa ya mafanikio yake? Pia kuhusu maisha yake binafsi maana ameoa miaka ya hivi karibuni, kuhusu Mama yake mzazi, mahusiono yake na Mama yake Naseeb, kazi yake kama actor na Dj, kulea mtoto wa mkewe na fame kwa ujumla. Tulikutana na tukazungumza hayo na zaidi.
Tafadhali enjoy.
 

Follow: