Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Shikana | DYNAMITE #Ep 17

SalamaNa Shikana | DYNAMITE

Mi na rafiki yanyu huyu tumepishana zaidi ya miaka kumi na nne, wakati anazaliwa mimi nilikua nagombana na makondakta kupata nafasi kwenye chai maharagwe ya kutoka Buguruni kuelekea Posta. Ila kupishana kwetu kwa umri naamini ndo kunaufanya ushoga wetu uwe special zaidi, maana yeye akiwa ananikhadithia kinachokiki kwenye umri wake, nami nakua namuelezea challenges za unapozidi kukua na naamini hii inatufanya tuwe bora zaidi. Na ki ukweli mara nyingi yeye amekua shujaa wangu, maana kuna mengine mazito kwake yanakua mepesi tu na hunisaidia kuona mambo kwa picha tofauti. Kwa hilo namshukuru sana. Wakati mwengine wanasema umri sio kipimo cha busara, rafiki yangu huyu kupitia mengi, kwahiyo moyo wake wa ‘chuma’ unatusaidia wengi kwenye kuweza kupambana na dhurba mbali mbali. Hapa sina haja hata ya kukuambia alipitia mitihani kiasi gani maana dunia nzima inajua, ila naweza tu kukuambia kwamba hakuna binti mwenye moyo wa utayari na ambae hana uwoga pale anapokua anasimamia lake kama Elizabeth Michael Kimemeta. Kwanza akiweka nia kwenye jambo lake lazima liwe... Atafunga, atakesha asali, ataweka akili na mawazo yake yote humo mpaka Mwenyezi Mungu amtimizie, nishashuhudia hilo sio mara moja wala mbili na naweza nikasema binafsi ameni inspire sana kwenye suala zima la funga na sala. Nani kamfundisha hayo? Kwa umri wake aliokua nao wakati matatizo mazito yalipomfika pengine usingedhani angekua binti wa dizaini hiyo. Miaka minne au mitano ambayo Alikutwa na yale matatizo ya kesi na mpaka akatumikia kifungo ni miaka ambayo ilimfaya akue sana. Ki imani na kiakili. Kwenye kipindi hiki hakua bado tayari kuzungumzia usiku ule ulobadilisha maisha yake ila kaniahidi akiwa tayari basi atafiria kutushirikisha kwenye hayo maongezi ila inawezekana pia hiyo siku isifike, nna hisia hiyo ni kurasa ya kwenye kitabu ambayo amechagua kuiruka kwa sasa au pengine milele, na maamuzi hayo mimi na wenzangu tuliyaheshimu. Sote tunakumbuka wakati anakua, kila kukicha yuko kwenye gazeti ila kwa sasa huyo si yule, amekua ki mwili, ki akili na hata ki sanaa pia. Mambo yake si ‘hadharani’ tena kama ilivyokua miaka ya nyuma. Sasa amekua influencer ambaye kampuni kubwa kadhaa zinamuamini yeye kuwatangazia biashara yao. Amekua Mama kwa mdogo wake Eric ambaye naye tumemuona akikua kwenye macho yetu. Mama kwa watoto wawili ambao amewakuta wakiwa wanaishi na mchumba wake nyumba moja. Kwenye haya maongezi yetu tuligusia hilo la hao watoto, na watoto wengine, kazi, yeye kama binti ambae amekua akikutana na mawe mengi. Muonekano wake. Familia kwa upande wa Mama na Baba na mambo mengine kadhaa. Niko hapa kukutakia uangaliaji mwema wa kipindi hiki na yangu matumaini utavutiwa na jambo ambalo litakufanya ubadili maisha yako kwa uzuri zaidi. Tafadhali enjoy.