Category

Mziki Mzuri App

Listen SalamaNa Monalisa | MASHHURA #Ep 19

SalamaNa Monalisa | MASHHURA #Ep 19  

Kabla sijasema jinsi ambavyo nampenda na kumheshimu mgeni wetu wa wiki hii napenda kusema cha kwanza ambacho nilikipenda kwake kwanza ilikua jina lake, Ms Yvonne Cherrie kisha Monalisa. Rafiki mzuri, mstaarabu na mtu mwema sana. Mona pia ana bahati sana, bahati ya kuwa na Mama ambaye ni hodari na mcheshi ambaye nae alifanya kazi yake ya kuhakikisha bintiye kwanza anafanya yote anayostahili kufanya kama mtoto kabla haja mshika mwanaye mkono na kumtambulisha kwenye dunia ya sanaa ambayo ilitufanya tumtambue na kumpenda pia na pia kuwakubali zaidi kama Mama na mtoto ambao ni mahodari sana. Kwenye kikao chetu hiki ambacho kilifanyika wakati Corona imependa moto na ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan Mona hakutusumbua kabisa, alitaka tu kupata uhakika wa usalama eneo la tukio na alikua pale on time kabisa, na pengine sisi inawezekana tulimsumbua kwa kutopokea simu kwa wakati. Mimi na Monalisa tunajuana kitambo kiasi so mazungumzo yetu yalianzia siku zile tulipokua tunaonana karibia kila siku, enzi za utoto wetu. Yeye alikua msanii hodari lakini pia alikua mmoja ya watangazaji mahiri kabisa wa Radio One na hata ITV. Enzi za kuwa ukurasa wa mbele wa magazeti ya udaku karibia kila Ijumaa na Jumatatu. Tulianzia hapo. Sote tunajua alipitia mambo meeeengi sana maskini ya Mungu, kuanzia maisha hayo ya umaarufu wa kuuza gazeti, mahusiano yake na Marehemu Meddy Mpakanjia na Amina Chifupa. Sanaa yake ya awali, ndoa yake na Marehemu George Tyson. Watoto wake, mahusiano yake na Mama yake, elimu, kazi na Sanaa kwa ujumla. Nilikua na wakati mzuri sana wakati tunarekodi hii na yangu matumaini pia uta enjoy.